NI BAADA YA SHOO YAKE NCHINI NIGERIA
Na Andrew Chale
MBUNIFU mkongwe wa mitindo nchini, Asia Idarous Khamsin kufuatia kufanya vizuri hivi karibuni katika onyesho kubwa la mavazi ya ubunifu lililokuwa maalum kwa ajili
ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,
lililofanyika Abuja, Nigeria, huku asilimia kubwa kwenye jukwaa hilo
akitumia vazi lililonakshiwa alama
za bendela ya Tanzania, ‘National colours Asia idarous’s design’ tayari
watu mbalimbali duniani wameombwa kutengenezewa mtundo huo.
Akizungumza
jiini Dar es Salaam, na mtandao huu, Asia Idarous ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Fabak Fashions, alisema kuwa watanzania na raia mbalimbali
wa kigeni duniani
kote wametoa order za kutengenezewa vazi kama hilo ambalo kwa asilimia
kubwa limekuwa ni kivutio huku likimweka mtu yoyote katika hali ya ubora
na kupendeza.
Vazi
hilo ambalo linabamba ikiwemo aina ya kitambaa maalum na skafu kubwa
inayopachikwa kifuani yenye nakshi ya alam za Taifa, pia tokea kuwekwa
kwenye mitandao ya kijamii na kwenye televisheni nchini Nigeria na
Ulala, imekua gumzo kubwa kwa sasa huku wengine wakishahuri liingizwe
kwenye tukio la kusaka vazi la Taifa.
“Kwa sasa nipo katika kushughulikia oda
za wateja wangu ambao wengi wapo Mataifa ya kigeni ikiwemo Nigeria,
Ghana, Kenya, uingereza, Marekani na kwingineko pamoja na Tanzania”
alisema Aisa Idarous.
Alisema
kuwa, vazi hilo ambalo pia siku ya onyesho hilo karibu wageni wote
wakiwemo balozi wan chi zaidi ya 61 zilizohudhulia siu hiyo ya Muungano
nchini Nigeria, zilivutiwa na hata kulipongeza kutokana na ua kielelezo
cha Utaifa la Tanzania.
Aidha,
Asia Idarous alisema kuwa, matilio ya vazi hilo yapo yanayotoka nchini
Tanzania namengine nje ya nchi ikiwemo Nigeria, tayari baadhi hoda zimekamilika na baadhi ameanza kuziuza katika duka la Fabak fashions lililopo Mikocheni mkabara na Kwa Mwalimu Nyerere.
“Hii ni heshima kwangu na kwa Tanzania, kwani vazi hili limeokea kukubalika duniani kote na kupelekea kuwa utambulisho maalum wa Mtanzania. Vazi hili kwa kawaida anavaa mtu yoyote na kwenye tukio lolote lile na hata kumweka mtu katika hali ya umaridadi, ikiwemo kwa wanaume na wanawake” alisema Asia Idarous.
Asia Idarous pia aliwataka kwa watu watakao taka kuagiza ama kutoa order, wanaweza kumpigia +255713263363, ama dukani kwake Fabak fashions Mikocheni kwa Mwl. Nyerere.







0 comments:
Post a Comment