Sammisago MrInfo Nimebahatika kufanya interview na stars wa Muziki kutoka Africa Kusini ‘Mafikizolo’ usiku wa kuamkia 5/April/2014 kuhusu ujio wao Tanzania na jipya wanalotaka kufanya hapa bongo.
Mafikizolo wamethibitisha kuwa Wanampango wa kufanya kazi na msanii
mkubwa kutoka Tanzania atakaye Tajwa hivi karibuni na colabo hii ndio
chanzo cha kuboresha mahusiano mazuri na wasanii wa Tanzania.
Kundi hili pia lina mpango wa kufanya video ya wimbo wao mpya
‘Nakupenda’ hapa Tanzania kabla ya kuondoka. Wanasema “Tungependa
kufanya video ya Nakupenda hapa Dar kwani jina la wimbo ni la kiswahili
na itapendeza hivyo, bado hatujapata director wa kufanya video hii ila
ndio mpango wetu’ .
Ni kawaida ya @SammisagoMrInfo kutoa habari exclusive kwa ajili yako,
Jipya kutoka kwa Mafikizolo ni kuhusu mabadiliko ya muziki wao,
Nhlanhla Nciza ameniambia kuwa “mabadiliko ya muziki wao yalifanyika ili
kuteka soko la bara lote la Africa na zaidi ikiwezekana ndio maana Khona na Happiness zina miondoka tofauti”.
Mafikizolo walikaa kimya bila kutoa album ya pamoja kwa muda wa miaka 4 na album yao mpya ya Mwaka 2013 iliyopewa jina Reunited ina muziki tofauti sana na muziki uliowahi kufanywa na kundi hilo.
SOMA ZAIDI: Fahamu | Sammisago







0 comments:
Post a Comment