Na Hassan Hamad, OMKR.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema
Watanzania wana kila sababu ya kusherehekea miaka 50 ya Muungano
kutokana na mafanikio yaliyopatikana.
Ametaja
baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni pamoja kuimarika kwa hali ya usalama,
ushirikiano na maelewano kwa wananchi wa pande mbili za Muungano.
Maalim
Seif ametoa kauli hiyo katika hafla ya mkesha wa miaka 50 ya Muungano
ilivyofanyika viwanja vya Mnazimmoja jijini Dar es Salaam, ambapo mgeni
Rasmi alikuwa Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda.
Amesema
miaka 50 tangu kuasisiwa kwa Muungano huo ni kipindi kirefu cha
kujivunia, ikilinganishwa kuwa nchi nyingi za Afrika zilizojaribu
kuungana zimeshindwa baada ya kipindi kifupi cha miungano yao.
Hata
hivyo amesema Muungano wa Tanzania bado unakabiliwa na kero nyingi
zinazohitaji kupatiwa ufumbuzi kwa maslahi ya pande zote mbili na vizazi
vijavyo.
Hafla
hiyo iliyoambatana na urushaji wa fashifashi, ilihudhuriwa pia na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi
0 comments:
Post a Comment