Ni mmoja kati ya wasanii kutoka Afrika Mashariki Judith Wambura a.k.a Lady Jay Dee
amepata ‘shavu’ la kuimba katika wimbo wa Kombe la Dunia mwaka
2014(FIFA World Cup Anthem 2014) akiwa yupo na wasanii wengine kama
David Correy kutoka Brazil na Rapper Octoppizo kutoka Nchini Kenya.
Katika hiyo ngoma Lady Jay Dee na David Correy wameimba kwa kutumia
lugha ya kiingereza huku Octoppizo akiwa amerap kwa lugha ya kiswahili.
Wimbo huo ambao umetambulishwa na Kampuni ya Coca Cola wakiwa wanazindua promosheni yao ya Kombe la Dunia itakayowezesha wateja wao kujishindia zawadi mbalimbali.
Jinsi Lady Jay Dee alivyopata shavu hili:
“Tuliweza kushiriki Coke Studio mwaka jana na nyimbo mbalimbali tulikuwa tunafanya zikiwemo nyimbo zetu wenyewe na zingine za copy,
na moja kitu tulichofanya ni kurekodi wimbo kwa ajili ya Kombe la
Dunia, kwa hivyo tulikuwa wasanii wengi mbalimbali wengine kutoka
Nigeria,South
Afrika, Tanzania, Uganda na Kenya, kwa hivyo baada ya hapo tulikuwa
tunasubiri huu wimbo uweze kutoka, na hatukufanyiwa audition ni wasanii
walewale tuliochaguliwa kutoka nchi nane za Afrika, kwenda kule ndiyo
tukarekodi baada ya hapo kikatoka kilichotoka, na ni wimbo mzuri ambao
umechangamka na unaongelea tu kuhamasisha watu kuhusiana na soka na vitu
kama hivyo”. Lady Jay Dee
SOURCE: Fahamu | Sammisago
SOURCE: Fahamu | Sammisago







0 comments:
Post a Comment