Saturday, April 26, 2014

Baada ya P-Square kumaliza tofauti zao, kaka yao amvisha pete ya uchumba mrembo wake

Dhoruba kali lililoitikisa meli ya kundi la P’Square linaloundwa na mapacha wa Nigeria, Peter na Paul Okoye limetulia na sasa mambo ni shwari kama zamani.
Utulivu huo umewekwa wazi na mapacha hao kupitia twitter kwa kueleza kuwa kundi hilo sasa liko imara zaidi ya siku zote.
Jana (April 24) ilikuwa siku ya kuzaliwa ya kaka yao, Jude Okoye na yeye alionesha nia ya kutaka kufunga pingu za maisha baada ya kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake lfy Umeokeke ambaye ni mwanamitindo na aliwahi kuvaa taji la urembo unaohusu masuala ya kijamii mwaka 2012.


Credit: timesfm

0 comments:

Post a Comment