Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Dk. Servacius Likwelile
akibadilishana mikataba ya makubaliano na Mkuregenzi Mkazi wa KfW Ofisi
ya Dar es Salaam.
Picha na Hussein Makame, MAELEZO
Hussein Makame, MAELEZO
SERIKALI
ya Tanzania na ile ya Shirikisho la Ujerumani zimesaini makubaliano ya
msada wa Fedha za Ulaya EURO Milioni 55.5 sawa na Shilingi Bilioni
121.89 za Kitanzania kusaidia sekta ya Maji, Umeme na Hifadhi ya Taifa
ya Serengeti.
Akizungumza
baada ya utiaji saini huo uliofanyika Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Uchumi Dk. Servacius Likwelile alisema katika makubalianao ya kwanza
Serikali ya Ujerumani itatoa EURO Milioni 20.5 sawa na Shilingi Bilioni
45.059.
Alisema
fedha hizo zitatumika kusaidia Kuhifadhi wa Hifadhi ya Serengeti katika
Kuendeleza na Kutunza maliasili ya hifadhi hiyo, kuboresha miundombinu
ya kijamii na kujenga barabara katika wilaya za Loliondo na Srengeti.
“Mkataba
wa makubaliano wa pili utawezesha Serikali ya Ujerumani kutoa mchango
wa EURO Miloni 20 sawa na Shilingi Bilioni 43.96 kusaidia kusambaza
umeme Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania “ alisema Dk. Likwelile.
Alisema
msaada huo utasaidia kuunganisha wananchi wa vijijini 32,500 katika
maeneo hayo kupata umeme na kuunganisha Gridi ya Taifa hadi kwenye
Mtambo wa Kuzalisha Umeme wa maji wa Rusumo na kuuza umeme nchini Rwanda
na Burundi.
Dk.
Likwelile aliongeza kuwa mkataba wa makubaliano wa tatu utaiwezesha
Serikali ya Ujerumani kutoa msaada wa EURO Milioni 15 sawa na Shilingi
Bilioni 32.97 kusaidia Sekta ya Maji kupitia Programu ya Maendeleo awamu
ya pili.
Alifafanua
kuwa kupitia programu hiyo msaada huo utafabikisha utekelezaji wa
Usimamizi wa Rasilimali ya Maji, Usambazaji wa maji Vijijini na Mijini
na Kuimarisha Taasisi na Kujengea Uwezo Sekta ya Maji.
Aliihakikishia
Serikali ya Ujerumani kuwa fedha hizo zitatumika vizuri na kuwanufaisha
wananchi wa maeneo husika na aliwaomba wanachi husika wathamini msaada
huo kwa kutunze miradi ya maendeleo katika maeneo hayo.
Balozi
wa Ujerumani nchini Tanzania Hans Koeppel msaada huo unathibitisha kuwa
Serikali yake imedhamiria kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo ili
kuchangia kuboresha ustawi na utajiri wa wananchi wa Tanzania.
Naye
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Modestus Lilungulu alisema msaada huo
utasaidia kutekeleza Mkakati wa Matokeo Makubwa Sasa ambao lengo lake ni
kufikisha huduma ya maji vijijini kwa asilimia 74 na mijini asilimia 90
ifikapo mwaka 2015.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Tanzania (TANAPA)
Allan Kijazi alisema kuwa msaada huo umekuja kwa wakati muwafaka
kutokana na changamoto ya ongezeko la idaidi ya watu lililosababisha
kuongezeka kwa huduma kwa binadamu kuongezeka.
Kwa
zaidi ya miongo mitano iliyopita Ushirikiano kati ya Serikali ya
Tanzania na Ujerumani umefanikisha misaada yenye thamani ya Fedha za
Ulaya EURO Bilioni 2.03 huku Serikali ya Ujerumani ikisaidia sekta za
Umeme, maji, mazingira na Afya







0 comments:
Post a Comment