
Meneja wa Shamba la zao la zabibu lililopo Chnangali, Wilaya ya
Chamwino mkoani Dodoma, Ronaldaka akisoma taarifa ya shamba hilo,
Washiriki wa semina ya Wenyeviti wa CCM kutoka kata za wilaya ya
Kinondoni, mjini Dar es Salaam, walipotembelea shamba hilo, jana kujua
zao za zabibu linavyozalishwa, changamoto na faida za kilimo cha zao
hilo.


Meneja wa shamba akiwaonyesha mfumo wa maji unavyofanya kazi kuyavuta
kutoka visimani kabla ya kumwagiliwa shambani. Wasita kushoto ni
kiongozi wa msafara huo, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Mzee
Madenge



Wajumbe wakionyeshana kitu wakati wakitazama bwawa maalum la maji ya kumwagilia mashamba ya zabibu

Meneja huyo akiwaonyesha wajumbe maji yanavyoingia kwenye vishina vya miti ya zabibu



Meneja wa shamba akimpa maelezo mkuu wa msafara mzee Madenge. Kulia
aliyevaa kijani ni Katibu wa CCM, wilaya ya Dodoma mjini Saad Kusilawe.
Wenyeviti wa CCM katika kata 31 za wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es
Salaam, wapo mkoani Dodoma kwenye semina au mafunzo ya siku nne kwa
ajili ya kujinoa zaidi weledi wao katika masuala mbalimbali ya kijamii
na uongozi. Imetayarishwa na theNkoromo Blog
0 comments:
Post a Comment