Saturday, November 2, 2013

Miaka 30 jela, viboko 12 kwa ujambazi

MKAZI wa Makongorosi wilayani Chunya mkoani Mbeya, Januari Juma (30) amehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela na kucharazwa na viboko 12 baada ya kupatikana na kosa la ujambazi wa kutumia silaha.
Adhabu hiyo iliyotolewa kwa Januari inatokana na kukiri mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wilayani Sumbawanga mkoani hapa, Adamu Mwanjokolo kuwa alitenda kosa la kupora pikipiki , simu ya mkononi na fedha taslimu kiasi cha Sh 45,000.
SOMA ZAIDI: HABARILEO ONLINE

0 comments:

Post a Comment