Wananchi wa Kijiji cha Ntunduru, Kata ya Isansa, wilayani Mbozi, Mbeya,
wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (hayupo
pichani) katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo leo, huku
wakiwa wamejikinga mvua kwa kutumia viti.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), Katibu wa NEC,Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro (wa pili kulia), Mwenyekiti
wa CCM, Mkoa wa Mbeya, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki,
Godfrey Zambi (wa tatu kulia) pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye wakipanda miti katika Zahanati mpya ya Ntunduru,
Kata ya Isensa, wilayani Mbozi, wakiwa katika ziara ya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na Kinana wakitoka kwenye nyumba ya
Balozi wa Shina la CCM, katika Kijiji cha Ntunduru, Mbozi, ambapo
alizungumza na wanachama wa shina hilo.
Kama kawaida yake, Kinana akishiriki katika ujenzi wa jengo la Zahanati ya Ntunduru
Kinana akiangalia moja ya vikundi vilivyokuwa vikitumbuiza alipofika katika Kijiji cha Ntunduru.
Kinana akimwangalia msanii wa sarakasi Huruma William anayefanya maajabu ya kutembea kwenye kamba
Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa kikundi cha Pa si Ilembo, Michael
Ilembo, aghani wimbo wa CCM alipotumbuiza katika mkutano wa hadhara
katika Kijiji cha Ntunduru, wilayani Mbozi.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ntunduru.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi, akihutubia katika
mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ntunduru, katika Kata ya Isansa,
Mbozi.
Kinana akivishwa mgolole na kupewa silaha za asili ikiwa ni ishara ya
kumsimika kuwa mmoja wa viongozi wa jadi wa kabila la Wanyiha, wilayani
Mbozi.
Kinana akiwasalimia wananchi alipokuwa akiingia kwenye mkutano wa
hadhara kwenye uwanja wa Stendi ya Malori, mjini Mbozi, ambapo
alihutubia na kusisitiza kuwa mawaziri mizigo hawatawaonea haya kuwasema
kwani hawawatendei haki wananchi na CCM pia.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro,
akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Mbozo, ambapo alisisitiza
suala la elimu kwa watoto pamoja na kupiga vita unyanyasaji kwa
wanawake.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye,akihutubia katika
mkutano wa hadhara mjini Mbozi, na kumtaka Waziri wa Kilimo, Ushirika na
Chakula kuacha tabia yake ya kila mara kuongea kwenye magazeti kwamba
Nape atumiea busara anapozungumzia matatizo ya utendaji wake kuhusu
matatizo ya wakulima nchini. Nape alisisitiza kuwa suala ya kumpeleka
Chiza kwenye kikao cha Kamati Kuu kujieleza halikwepeki. PICHA ZOTE NA
KAMANDA RICHARD MWAIKENDA
KATIBU wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amemtaka Waziri
wa kilimo, Chakula na Ushirika kuacha kumshambulia kwenye vyombo vya habari na badala
yake atumie muda huu kuandaa majibu ya kuwasilisha mbele ya Kamati Kuu kutokana
na hoja zilizoibuliwa na wakulima nchini.
Akihutubia mamia ya wananchi wa mji wa Mbozi katika mkutano wa
hadhara uliofanyika jana wilayani hapa Nape, alionyesha kukerwa na tabia ya
Waziri Chiza kumshambulia kwenye vyombo vya habari kwa kwa maneno ya kejeli.
“Ndugu Katibu Mkuu tumezunguka wilaya nyingi nchini hakuna mahali ambako
hakuna malalamiko ya wakulima ambao ni asilimia 80 ya watanzania wote. Kutokana
na hali hii sasa tunamtaka waziri Chiza aje mbele ya CC mwezi ujao na kueleza
anatatuaje changamoto hizi.
“Yeye amekazana kila kukicha kunishambulia kwenye magazeti. Nataka
kumpa ushauri wa bure mheshimiwa sana
waziri, anachofanya hanishambulii mimi anawashambulia wakulima kwa sababu
siongei masuala yangu binafsi ila niongealea malalamiko ya wakulima,” alisema
Nape
Alisema amemvumilia kwa muda mrefu ila kwa sasa amechoka, ambapo kila kukicha Waziri huyo amekuwa akitumia
maneno ya kejeli na vijembe huku akimtataka kujifunza busara ya Naibu wake Adam Malima.
“Malima aliposikia wito wetu akasema yuko tayari kuja kujieleza
kwenye Kamati Kuu kwa kuwa chama ndiyo mwajiri wake hivyo atazingatia maamuzi ya
chama, yeye waziri kila kukicha Nape Nape Nape, kunishambulia hakuondoi kero za
wakulima.
"Nimesikia leo anasema sina busara!! busara ipi anayohoji? Mie
ninayewatetea wakulima wanaolalamika kulazimishwa kutumia mbolea ya Minjingu
inayounguza mazao yao
na yeye anayeleta mbolea hiyo na kulazimisha wakulima watumie nani anatumia
busara hapa.
“ Yeye anayepuuza malalamiko ya wakulima kuumizwa na baadhi ya
maafisa ushirika na mimi ninayetaka hatua zichukuliwe dhidi ya maofisa wake
nani anatumia busara??,” alisema na kuhoji.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment