Tumepokea taarifa za masikitiko
kuhusu vurugu zilizotokea huko Buselele Chato kuhusu uchinjaji wa nyama
unaobishaniwa na Waislam na Wakristo.
Chanzo cha Habari
hizi kimetueleza kuwa baada ya mivutano kuhusu uchinjaji wa nyama .Baaadhi ya
Wakristo waliamua kuanzisha bucha ya ili wachinje na kununua hapo ili
wasishiriki kula nyama zilizochinjwa kama sehemu ya ibada ya Kiislamu kwa vile
uchinjaji kwa Waislam ni ibada.
Baada ya kufungua
Bucha hiyo leo asubuhi taarifa inasema watu wanaosadikiwa kuwa waislam walifika
kutaka kuifunga hiyo Bucha na baadaye Polisi nao walifika na walitaka wamchukue
mwenye bucha hiyi .
Suala hili likazua
tafrani na pakatokea mapigano kati ya pande mbili yaani waislam na wakristo na
kuna watu wameumizwa.Taarifa imezidi kueleza kuwa pia mali za aliyehamasisha
ufungwaji wa bucha nazo zimeharibiwa. Baada ya kupokea taarifa hii tumewatuma
waangalizi wetu wa haki za binadamu kwenda kutuletea kwa kina hali halisi kama
watakavyoweza.
Tunahabari kuwa
kikosi cha kuzuia fujo kilifika na kutuliza hizo vurugu.Jambo tunaloliona kwa
haraka ni kuwa kunaelekea kukosekana kwa uongozi wa kuyatazama masuala kama
haya na kuyawekea msimamo na maelekezo kabla vurugu kama hizi kutokea.
Pili tunaona kuwa
hali ya kukosa stahamala za kidini inajengeka nchini jambo ambalo ni hatari
sana kwa usalama na amani hapa nchini.Wakati tunasubiri taarifa zaidi tunapenda
kutoa angalizo kwa viongozi wetu maana tumesikia mkuu wa wilaya tayari
ameshafika katika eneo la tukio.
Masuala kama haya
yatazamwe kwa mujibu wa sheria na sheria zifuatwe lakini pia kwa kuzingatia
haki za binadamu na hususani haki za kiraia na kiutamaduni ambazo zinatoa uhuru
wa ibada na kila mtu asiingiliwe katika haki hizi.
Lakini pia njia za
utatuzi wa migogoro ya aina hii isifanywe kijuujuuu bali pawe na nafasi
yamaongezi ya kina ya uchambuzi wa kiini cha mgogoro. Tutaweza kutoa taarifa
zaidi tutakapopokea taarifa kutoka kwa waangalizi wetu wa kiini na matokeo ya
mgogoro au vurugu hizi







0 comments:
Post a Comment