Thursday, January 31, 2013

ECOBANK SASA NA HUDUMA ZA KIBENKI BILA KUFIKA MATAWINI

Kwa Vyombo Vya Habari
Toleo la leo

Mawasiliano: Daisy Mumbi
PR Consultant
Ecobank Tanzania Limited
Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 765 936 325


(HUDUA ZA KIBENKI BILA KFIKA MATAWINI KUONGEZEKA TANZANIA)
Ecobank yaongeza ufanisi kwa upatikanaji wa huduma za kifedha Tanzania

Dar es Salaam, Tanzania - 31 Januari 2013 - Ecobank Tanzania Limited ambayo ni mojawapo katika  kundi la Ecobank Africa iliyo katika nchi 33 Africa, inashirikiana na Kundi la Ushauri wa Kusaidia Maskini (CGAP) shirika la kimataifa la makazi katika benki ya dunia, kuleta huduma za benki karibu na watu.

Akizungumza katika warsha ya Ecobank ya kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha katika Hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam ,Enoch Osei-Safo, Mkurugenzi Ecobank Tanzania alisema, "ushirikishwaji wa fedha itawapa watanzania urahisi kupata huduma za kibenki hasa kwa Watanzania ambao hawana huduma hizi. Hii ni dhana ambayo tunaendeleza ndani ya Ecobank Africa na hasa kwa Tanzania itarahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa watu wa kipato cha chini  ili kuendeleza uchumi wa nchi hii.”

Steve Rasmussen (Meneja wa Teknolojia na uvumbuzi wa biashara, CGAP), alionyesha furaha sana kwa ushirikiano wa pamoja wa Ecobank. Katika hotuba yake ya utangulizi, alisisitiza kuwa ushirikiano huu utajenga uwezo na kuandaa taasisi ya kuleta huduma za benki karibu na wananchi.

Patrick Akinwuntan;  Mkurugenzi Mtendaji,  wateja binansi na wajasiliamali, Ecobank Africa  katika mada yake alisisitiza kuwa Ecobank itaendelea na jitihada za kukuza njia mbadala kama sehemu ya mkakati wa kuleta huduma za benki kwa wananchi. "tunazo zaidi ya ATM 1, 600 katika mtandao, POS zaidi ya 4500, Ecobank Internet Banking na Ecobank MobileMoney.
Ecobank Tanzania imeweka kipaombele kuongeza upatikanaji wa  huduma za benki kwa Watanzania , hasa kulenga wakazi ambao wamekuwa wananyimwa kupata huduma za benki kutokana na gharama kubwa za uendeshaji wa akaunti ya benki na wale wanaoishi mbali na taasisi za kibenki.

Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.ecobank.com

# # #

Kuhusu Ecobank
Ecobank ni moja ya benki zinazoongoza katika  Afrika, pamoja na usambazaji wa nchi zaidi katika Afrika kuliko benki nyingine yoyote katika dunia. Ecobank inatoa huduma za benki balimbali.
Mtandao wa usambazaji katika Afrika ni pamoja na;
Benin, Burkina Faso, Burundi, Cameroon, Cape Verde, Jamhuri ya Afrika, Chad, Congo (Brazzaville), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ivory Coast, Gabon, Gambia, Ghana, Guinea, Guinea-Bissau, Kenya, Liberia , Malawi, Mali, Niger, Nigeria, Rwanda, Sao Tome na Principe, Senegal, Sierra Leone, Tanzania, Togo, Uganda, Zambia na Zimbabwe

Mtandao;
Ipo katika nchi 35 - ikiwa ni pamoja na nchi 32 za Afrika
Zaidi ya matawi 750
Zaidi ya ATM 800


 

0 comments:

Post a Comment