Friday, December 14, 2012

Stamina Kuachia Albam Yake Januari 2013




  
Rapper wa muziki wa kizazi kipya anayewakilisha Moro Town, Stamina anatarajia kuachia album yake mapema mwakani. Stamina , mkali wa ngoma kama Kabwela, Alisema, Najuta Kubalehe na nyingine nyingi, alisema mitaa ya Januari fans wategemee album yake hiyo ambayo itakuwa  kwenye mtindo au miondoko ya Hip-Hop ikiwa imeshiba Track 22 ndani yake.

Stamina ambaye chimbuko lake ni Morogoro, aliyasema hayo na kuongeza kuwa, album hiyo imeshirikisha wasanii kibao kutoka bongo, kama Rich Mavoko, Fid Q, Mtu Chee na wengine kibao.

Katika hatua ingine, Stamina alisema single yake mpya aliyomshirikisha Fid Q inayojulikana kama Moro Moro ambayo teaser yake ilishatoka, hii itafuata kuiachia kwenye media kwa ajili ya fans wake na ipo katika hatua za mwisho za kuimalizia kuitengeneza na kwamba wakae mkao kwa zigo hilo ambalo yeye mwenyewe anasema ni kali sanaaa.
 

0 comments:

Post a Comment