Wakati
wimbo wa Diamond ‘nataka kulewa’ ukizidi kufanya vizuri na kutengeneza topic
kwenye media kibao TZ na kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo wengi
wanasema beat hiyo inafanana asilimia 100 na ile ya beat ya wimbo wa Pasha
alomshirikisha Tunda Man ‘Mtoto Amekua’, Manecky wa AM records ambae ndiye
aliyetengeneza ‘nataka kulewa’ amesema beat ya wimbo huo ni tofauti kabisa na
ile ya wimbo wa Pasha....
Producer
huyo ambae ndiye mshindi wa kili music awards 2011 kama producer bora wa mwaka
alifunguka kwa msisitizo kwenye XXL cha Clouds fm kuwa hakusample beat sehemu
yeyote ile na hiyo beat aliifanya kwa mawazo yake mwenyewe kuanzia mwanzo
kabisa. Tena kwa kidhungu “from the scratch”.
Alipoulizwa
maoni yake kama beat hizo mbili zinafanana au hazifanani, alisema “kwa kitu
ambacho mimi nimeweza kusikiliza hizi ni beat mbili tofauti, sema kuna idea ya
lead sound ambayo inaweza kuwa na mfanano flani, ndio maana nikarudia kusema
palepale, mimi ni mtu ambae nasikiliza muziki kila siku, na ni binadamu na sio
computer sio kitu flani ambacho kinasema ni kitu flani kifanye hivi…!”
Manecky
amesema hata Tunda Man aliisikiliza ‘beat ya Nataka kulewa’ mara nyingi tu
lakini hakuweza kuifananisha kabisa na ile ya wimbo wa Pasha ambao yeye
mwenyewe kaweka vocal yake kwenye beat ileile inayofananishwa, lakini
inaonekana alipousikia watu wanasema zinafanana ndipo na yeye akashtukia kuwa
inawezekana iko hivyo.Duuuh..! Kweli tunatofautiana kushtukia copy, wengine
wakisikia hata kinanda cha kwanza tu wanashtukia ila Tunda Man yeye ameshtuka
baadae sana pamoja na kuitumia beat hiyo.
Wimbo wa Diamond umepata challenge
kubwa sana tangu au-release rasmi, muda mchache baada ya kuonekana beat
inafanana na ya wimbo wa Pasha ft. Tunda Man ‘nataka kulewa’, H-Baba
alijitokeza na kumtuhumu Diamond kwa kumuibia idea ya wimbo huo tena kwa
makusudi huku akiweka hadharani vielelezo vya demo ya wimbo wake ‘nataka
kulewa’ akiwa na Q-Chillah.







0 comments:
Post a Comment