SHINDANO la kumtafuta Mfalme wa Kurap Bongo lililoandaliwa
na Ukumbi wa Dar Live, litaanza Jumapili hii katika ukumbi huo uliopo Mbagala,
kikini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Atriums
iliyopo Sinza Afrika Sana, jijini Dar, Meneja Mkuu wa kampuni ya Global
Publishers Ltd ambao ndio wamiliki wa ukumbi huo, Abdallah Mrisho, amesema
mshindi atazawadiwa gari la kifahari ambalo litatangazwa hivi karibuni.
Kuanziakesho, vijajna wajitokeze pale Dar Livekwa wingi ili
kushiriki. Jumapili ya wiki ijayo ndiyo watapata nafasi ya kuonyesha vipaji
vyao, na mchakato mzima wa kumtafuta mshindi ndiyo utakuwa umeanza rasmi,”
alisema Abdallah.
Aidha, mratibu wa shindano hilo, Luqman Maloto, amesema watu
wajitokeze kwa wingi kwani hakuna ‘longolongo’
na majaji watakuwa watu wenye heshima kubwa kwenye gemu ya muziki Bongo pamoja
na wananchi watakaokuwa wakihudhuria Dar Live.
(PICHA/HABARI: ERICK EVARIST/GPL)
0 comments:
Post a Comment