Baada ya msanii wa
filamu bongo Hemed Suleiman ‘P.H.D’, kutangaza
endapo akiamua kuoa basi atafanya mchakato kama wa kufanya usaili kama
ilivyo BSS au mashindano mengine ili kufanya mchujo wa mwanamke mzuri
atakayekuwa mke wake, kauli hiyo imepingwa na mwanadada Jackline Pantezel ‘Jack
wa Chuz’, kwa madai kitendo alichokisema msanii huyo kinahitaji
awaombe msamaha wanawake kwani anawafananisha na samaki wanaovuliwa
kirahisi.
Kauli ya Jack imeonyesha wazi kuwa
anawatetea wanawake na hataki waonekane kama hawana maana yoyote ndani ya
jamii au watu wanaokaa na kusubiri kuolewa tu wakati maisha ya sasa hayapo
hivyo, na mwanamke yeyote atakaejitokeza kwenye mchakato huo atakuwa hana
akili na atakuwa ni kahaba.“Nilisikia tu kwamba anataka kufanya kitu kama BSS katika kutafuta mwanamke wa kuoa, na hapo ina maana kuwa tayari amesha wafanya wanawake kama samaki,” alidai Pentzel.
Hemed Suleiman 'PHD' |
0 comments:
Post a Comment