![]() |
Jaguar na Prezzo |
Katika hali inayoashiria kuwa beef kati
ya Msanii Prezzo na Jaguar wote wa nchini Kenya, Jaguar ameibuka na kumponda
Prezzo kuwa hana lolote katika muziki.
Jaguar ambaye jina lake halisi ni
Charles Njagua amesema kuwa Prezzo ni mwanamitimindo na sio mwanamuziki na
hivyo hawezi akashindana na yeye.
“Prezzo
sio mwanamuziki me namuona kama model kwakuwa ameshinda category ya Best
Dressed katika tuzo za Chaguo La Teeniez mara moja, basi hawezi
shindana na mimi kivyovyote” alisema.
Jaguar alisema kuwa hata linapokuja
suala la fedha hawezi akashindana nae kwa kuwa yeye ana mafanikio makubwa
kuliko Prezzo, alisema kwa sasa anamiliki
gereji ya kisasa inayoitwa Jagz Auto iliyopo mjini Nairobi, kampuni ya taxi
iitwayo Jagz cabs na kampuni ya ulinzi iitwayo Jagz Security.
“Prezzo hawezi kuongea kuhusu hela
kwasababu ntamuumbua katika kitengo hicho hasa pale tutakapoamua kutangaza mali
zetu" aliongeza.
0 comments:
Post a Comment