Usiku
wa kuamkia leo Msanii wa Bongo Movie Steven Kanumba amefariki dunia baada ya
kuangukia kisogo kwa kile kinachodaiwa kusukumwa na mpenzi wake Lulu. Kwa
mujibu wa mdogo wa msanii huyo alisema awali kulikuwa kuna mzozo baina ya
kanumba na Lulu ambapo waliamua kuingia ndani ili waweze kumaliza mzozo huo
lakini baada ya muda Lulu alitoka na kumuita mdogo wa Kanumba aje amuangalie
kaka yake ameanguka baada ya kuingia ndani na kumkuta kaka yake ameanguka
ilibidi aende akamuite daktari na aliporudi alikuta Lulu ameondoka.
Chanzo
cha mzozo huo inadaiwa kuwa ni Lulu kuongea na mwanaume mwingine kwenye simu
hali iliyopelekea kuzuka kwa mzozo huo.
Inasemekana
Lulu tayari ameshakamatwa na anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Osterbay.
REST IN PEACE OUR KAKA MKUBWA
STEVEN KANUMBA ‘THE GREAT’
0 comments:
Post a Comment